TIRA YATOA MISAADA HOSPITALI YA SOMANDA NA SHULE YA SEKONDARI BARIADI

 

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kupitia Kanda ya Ziwa na kwa kushirikiana na kampuni za bima tarehe 23 Agosti, 2024 walitoa misaada mbalimbali katika Hospitali ya Somanda na shule ya kutwa ya Bariadi, wilayani Bariadi, Simiyu.
Vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu vilitolewa  kama sabuni, taulo za kike, mipira, daftari n.k, pia Mkurugenzi  wa wilaya ya Bariadi Ndg. Adrian Jungu alikuwepo katika tukio hilo, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kenan Kihongosi. 
Baada ya utolewaji wa misaada hiyo, baadhi ya washiriki walipata nafasi ya kufanya kikao mkakati kuimarisha soko la Bima nchini.
Kanda ya Ziwa inahudumu mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera.

 

Related Posts