Risasi yaivuruga Veta | Mwanaspoti

TIMU ya Risasi imeifunga Veta kwa pointi 50-49 katika Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika Uwanja Veta mjini humo.

Kwa matokeo hayo, Risasi inashika nafasi ya pili kwa  pointi tisa, huku Kahama Sixers ikiongoza kwa pointi 10.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Shinyanga, kamishina wa Ufundi na Mashindano wa mkoa huo, George Simba alisema mchezo wa mwisho wa mzunguko wa pili kati ya Risasi na B4 Mwadui ndiyo utakaomua nani atashika nafasi ya kwanza.

Kwa mujibu wa maelezo ya Simba, timu itakayoshika nafasi ya kwanza itacheza na itakayoshika nafasi ya nne, huku  itakayoshika nafasi ya pili itacheza na ya tatu katika hatua ya nusu fainali. 

Related Posts