TAEC YAJIPAMBAMBANUA MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA KWA UKUSANYAJI WA MADUHULI YA SERIKALI.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akizungumza na waandishi na Wahariri kwenye Mkutano unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato  Kosuri akizungumza kuhusiana uratibu wa mikutano hiyo kwa Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina kizungumza juu ya Utendaji wake ili wananchi wajue ,jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahariri na waandishi wa habari katika Mkutano wa TAEC.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imesema katika Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan makusanyo ya maduhuli ya serikali yameongezeka kutoka sh.bilioni 8.7  mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia  sh. bilioni 10.9 mwaka wa fedha 2022/2023.

Akizungumza na waandishi wa habari na Wahariri jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Profesa Lazaro Busagala  amesema kuwa makunyanyo hayo yametoakana mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika utoaji wa huduma.

Amesema kuwa majukumu ya Tume ni mawili ambayo kudhibiti matumizi salama ya mionzi na kuikuinua matumizi salama ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Profesa Busagala amesema lengo ya matumizi salama ya miozi  ni kuhakikisha kuna usimamizi, udhibiti na uhamasishaji wa matumizi ya amani na salama ya teknolojia nyuklia hapa nchini.

Amesema kanuni zinazosimiwa na TAEC ni  Nguvu za Atomu za Kinga ya Mionzi Ionishi na Isiyo Ionishi za mwaka 2023, Kanuni za upakiaji na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi ya Mwaka  2011, Kanuni za Nguvu za Atomu za Udhibiti Wa Mionzi Katika Mnyororo wa Vyakula na Bidhaa Zinazohusiana na Chakula za Mwaka 2023.

Aidha amesema kanuni zina zinazosimamiwa na TAEC Kanuni ya usimamizi wa Mabaki ya Mionzi kwa Ulinzi wa Afya ya Binadamu na Mazingira

Amesema TAEC ina majukumu kusimamia na kudhibiti  matumizi salama ya mionzi.

 Profesa Busagala amesema  TAEC inatoa lesseni kwa wale wote wanaomiliki vyanzo vya mionzi baada ya kutimiza masharti ya kiusalama wa mionzi na nyuklia.

Amesema TAEC inahamasisha na kuendeleza  matumizi salama ya sayansi na teknolojia ya nyuklia pamojà na kuratibu miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo mbalimbali hasusani shirika la nguvu za Atomu la kimataifa (IAEA) na Umoja wa Ulaya na wadau wengine.

   Hata hivyo amesema  TAEC inatoaa vibali vya uingizaji, umiliki, na utumiaji wa vyanzo vya mionzi ,Kukagua vituo vyote vyenye vyanzo vya mionzi ili kuweka usalama na kinga ya mionzi kwa wananchi na mazingira , kukagua ubora wa mashine ya uchunguzi wa magonjwa CT-SCAN,Kudhibiti madhara ya mionzi kwa kupima kiwango cha mionzi kwenye minara ya simu na rada za mawasiliano.

Profesa Busagala amesema katika kazi zingine zinazogisa maisha ya afya ni udhibiti usalama wa mnyororo wa vyakula kwa kupima sampuli za vyakula, mbolea, vyakula vyawanyama, mazao

pamoja vinavyoingizwa na kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa TAEC  wanapima sampuli za mazingira ili kubaini uchafuzi wa mionzi kwenye mazingira hivyo kudhibiti madhara ya mionzi,Kudhibiti madhara ya mionzi kwa kutoa huduma ya upimaji wa mionzi kwa wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye maeneo yenye vifaa vya mionzi, Kukusanya, kusafirisha na kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi ili kuepuka kuhatarisha maisha ya wananchi.

Amesema kuwa  Wanaratibu miradi mbalimbali inayotumia teknolojia ya nyuklia hapa nchini ikiwemo upatikanaji wa maji Makutupora kwa ajili ya jiji la Dodoma mwaka 1979 mpaka 2001,Kuendesha kituo cha kupima uchafuzi wa anga unaotokana na majaribio ya silaha za nyuklia.

Amesema kuwa wanaendeleza tafiti za teknolojia ya nyuklia

maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii

Serikali imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga miundo mbinu inayoipa TAEC uwezo wa kutoa huduma kwa tija na ufanisi.

Hata hivyo amesena Serikali imejenga majengo 6 ya maaabara na ofisi katika kanda 5 yenye thamani ya takribani Bilion 28.11 ambapo majengo 4 kati ya hayo yamekamilika ambayo iko Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.

 Katika kusogeza huduma katika Kanda pamojà na Zanzibar 

Ziwa (Mwanza)

Makao Makuu (Dodoma)

Mashariki (Dar es Salaam)Zanzibar

Kaskazini (Arusha) huku  wakiwa na  Ofisi 63 na Zanzibar kwenye Kanda 6 Makao Makuu Dodoma Kaskazini – Arusha Mashariki – Dar es Salaam ,Ofisi ya Zanzibar – in Unguja ,Kanda ya Ziwa – Mwanza,Nyanda za Juu Kusini – Mbeya

Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea na jitihada za kuwasogezea wananchi huduma karibu na maeneo yao kwa kufungua ofisi. Katika miaka mitatu ofisi 14 zimefunguliwa na kuwekewa vitendea kazi, hivyo kuzifanya kuwa 63 mipakani, mikoani lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi hivyo kuinua shughuli za kiuchumi za wananchi.

Amesema  Serikali ya awamu ya Sita kufungua ofisi za kanda, mipakani na kutumia mifumo ya TEHAMA kama vile TANCIS, TeSWS na EDMS katika kutoa huduma

Profesa Busagala amesema katika mafanikio mengine ni  kupunguza siku za utoaji wa cheti cha uchunguzi wa mionzi (RAC) kutoka zaidi ya siku 7 hadi kufikia kwa wastani wa masaa 3 hadi siku moja kwa asilimia 98 na maombi yake ni Kwa kutumia mfumo wa kielektroniki hali iliyosaidia kupunguzavmalalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali.

Related Posts