MITAA iliitika mitaa ikaukubali mziki wa Magwiji wa Odds kubwa, Nyumba ya Mabingwa wa
michezo ya ubashiri na kasino ya mtandaoni, ufalme wa washindi Meridianbet pale
walipopita mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na kuwashika mkono
wapambanaji wote.
Watu wengi walijitokeza kuona ni nini
Meridianbet wamewaletea na hapo ndipo tabasamu lilipofunguka mithili ya jua la
asubuhi linavyochomoza, mitaa na chocho zote za Jiji la bata na salama,
liliguswa kwa kupatiwa nguo za kujikinga na mvua kwa Bodaboda na abiria wote,
wafanyabiashara mbalimbali nk
Kwa niaba ya madereva bodaboda na bajaji
muwakilishi wao aliyefahamika kwa jina moja la Athuman alisema “Meridianbet
hakika ni mwanga wa kila mtu na leo kila mtu anafaidika na msaada huu”
Meridianbet imetoa msaada wa nguo za
kujikinga na mvua kwa madereva Bodaboda na Bajaji, wafanyabiashara wa sokoni
ikiwa ni sehemu ya kupambana na madhara yatokanayo na mvua zinazoendelea
kunyesha katika Jiji hili la Dar Es Salaam. Kwa upande wa muwakilishi wa
Meridianbet alisema kwamba;
“Kampuni inatambua mchango wa madereva
hao, na hivyo wameamua kuunga juhudi zao kwa kutoa msaada wa nguo hizo ili
kutoathiri kazi yao kipindi mvua inaponyesha, pamoja na madhara ya kiafya
yatokanayo na kunyeshewa na mvua”
Meridianbet ni kampuni inayofanya
shughuli za ubashiri mitandaoni, na michezo ya kasino
ya mtandaoni,
kila siku washindi wengi wanajizolea mamilioni na kutajirika, pamoja na yote
hurudisha kwa jamii kile wanachokipata.