Diwani na wenzake 10 washtakiwa kwa kuingia Msitu wa Kilombero, watupwa mahabusu

Kilombero. Diwani wa kata ya Mbingu iliyopo Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Nestory Peter na wenzake 10 wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya msitu wa asili wa Kilombero (KNR).

Katika kesi hiyo namba 24675/2024, Wakili wa Serikali, Dastan William amewasomewa shtaka hilo washtakiwa wote kwa pamoja mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Regina Futakamba.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili William amedai kuwa mshtakiwa wa kwanza, Nestory Peter ambaye ni diwani wa Kata ya Mbingu na wenzake 10 walikutwa ndani ya msitu huo Agosti 26, 2024 wakitenda kosa hilo jambo ambalo ni kinyume cha kisheria.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa wote wamekana kufanya kosa hilo na Hakimu Futakamba ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, 2024 itakapotajwa tena mahakamani hapo na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi kuhusu mwenendo wa kesi hii.

Related Posts