Hakujawa na uthibitisho wa mara moja kutoka kwa upande wa Wapalestina kuhusu kifo cha Mohammed Jaber, aliyejulikana kama Abu Shujaa, kamanda katika Kundi la wanamgambo wa “Islamic Jihad” katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams huko nje kidogo ya mji wa Tulkarem.
Anatazamwa kama mtu shujaa kwa Wapalestina wengi, baada ya mwaka huu kuripotiwa kuuwawa katika operesheni moja ya jeshi la Israel, lakini baadaye akaushangaza umma wa Wapalestina pale alipoibuka kwenye mazishi ya wanamgambo wengine, ambapo alibebwa juu, juu mabegani na umati wa watu waliokuwa wakimshangilia.
Israel ilifanya operesheni kubwa katika Ukingo wa Magharibi usiku wa kuamkia Jumatano. Hamas ilisema wapiganaji wake 10 waliuawa katika maeneo tofauti, na Wizara ya Afya ya Palestina iliripoti majeruhi 11, pasipo kusema kama walikuwa wapiganaji au raia.
Pendekezo la kuwekewa vikwazo mawaziri wa Israel
Katika hatua nyingine Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell Borrell, amewasilisha pendekezo lake kwa Umoja wa Ulaya la kuwekewa vikwazo maafisa waandamizi wa serikali ya Israel. Vikwazo vilivyopendekezwa vinamlenga Waziri wa Fedha wa Israel Bezaleli Smotrich na Waziri wa Usalama waKitaifaItamar Ben-Gvir.
Shirika la habari la Ujerumani DPA limefanikiwa kulipata pendekezo hilo ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kukuta wa leo hii kwa ajili ya mazungumzo ambayo yanajikitia pamoja na mapigano ya Gaza, kadhalika Ukraine na uchaguzi uliozusha utata wa Venezuela.
Kauli tata za viongozi wa Israel
Wote kwa pamoja Smotrich na Ben-Gvir hivi karibuni walitoa kauli ya kuudhi dhidi ya Palestina. Ni washirika wa muungano wa mrengo wa kulia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Lakini pia wawili hayo ni watetezi wa sera ya makazi katika maeno ya ulowezi, ambayo mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa inaona kuwa ni kinyume cha sheria.
Hivi karibuni Ben-Gvir alitoa wito wa kukomeshwa kwa utoaji wa misaada huko Gaza Ukanda kwa lengo la kutoa mbinyo zaidi kwa wanamgambo wa Hamas. Smotrich alitoa taarifa kama hiyo, akipendekeza kizuizi kinachowezekana cha misaada hadi mateka wote wa Israel waliokuwa wanashikiliwa na Hamas waachiliwe.
Soma zaidi: WFP lasitisha harakati Ukanda wa Gaza
Yeye alionesha hatua hiyo ni njema kiutu, hata kama inaweza kuhatarisha maisha ya watu milioni mbili ambayo kwa sasa ipo katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza. Baada ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7, inaaminika kwa wakati huu kundi hilo linawashikiliwa mateka 107, ambapo theluthi ya hao inawezekana kuwa wameuwawa.
Vyanzo: AFP/DPA