WAKATI Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi kushika kasi, mchuano umehamia kwa timu zitakazoshuka daraja kazi ikiwa kwa timu tano zinazochuana zisishuke.
Timu hizo ni KIUT yenye pointi 30, Jogoo (28), Ukonga Kings (27), Crowns (27) na Chui (25), zipo katika mtihani huku tatu kati ya hizo ndizo zitakazoshuka daraja.
Zitakazoshuka daraja zitajulikana pale kila timu zikishacheza michezo 30.
Wakati timu hizo zikichuana katika vita ya kushuka daraja, timu zilizopo katika nafasi ya kucheza hatua ya nane bora ni Dar City yenye pointi (48), UDSM Outsiders (48), Savio (45), na JKT (42).
Nyingine ni Mchenga Star yenye pointi 40, Vijana ‘City Bulls’ (39), ABC (38), Srelio (36), DB Oratory (35), Pazi (32) na Mgulani JKT (31) kati ya hizo zitaungana na timu nne za juu.
DB Troncatti yaendelea kukimbiza
IKIWA zimesalia michezo minne kwa baadhi ya timu kabla ya kumalizika kwa duru la pili la Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), DB Troncatti inaendelea kuongoza kwa upande wa Wanawake ikiwa na pointi 49 katika msimamo wa ligi hiyo.
Timu inayoifukuzia kwa karibu ni Pazi Queens iliyopo nafasi ya pili ikiwa na pointi 45, huku Tausi Royals ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 44.
Vijana Queens (43), Jeshi Stars (41), DB Lioness (41), JKT Stars (40),Polisi Stars (38) na Mchenga Stars (35).
Zingine ni City Queens (34),Ukonga Queens (32), Mgulani Stars (30), Twalipo Queens (29), UDSM Queens (28), Kigamboni Queens (27) na Kurasini Divas (23).
TIMU PL W L PTS
DB Troncatti 26 3 3 49
Pazi Queens 26 19 7 45
Tausi Royals 24 20 4 44
Vijana Quees 23 20 3 43
Jeshi Stars 23 18 5 41
DB Lioness 25 16 9 41
JKT Stars 21 19 2 40
Polisi Stars 25 13 12 38
Mchenga Queens 25 10 15 35
City Queens 25 9 16 34
Ukonga Queens 25 7 18 32
Mgulani Stars 22 8 14 30
Twalipo Queens 24 5 19 29
UDSM Queens 26 2 24 28
Kigamboni Queens 25 7 18 27
Kurasini Divas 22 3 17 23