PLANET imeonyesha ubabe kwa kuifunga timu ngumu ya Eagles kwa pointi 62-59 katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mirongo, jijini humo.
Mchezo huo ni wa pili kwa timu hiyo kupoteza katika mchezo wa kwanza iliweza kufungwa na Planet kwa pointi 81-72.
Mchezaji Romanus wa Planet aliongoza kwa kufunga pointi 17, alidaka mipira ya ‘Rebounder’ mara saba, aliiba mipira kwa mpinzani (steal) mara saba na asisti alitoa kwa wachezaji wenzake mara tatu.
Kwa upande wa Eagle, mchezaji Lubago alifunga pointi 15, akidaka mipira ya ‘rebounder’ mara mbili akitoa pia asisti tatu na aliiba mipira (steal) mara mbili.
Katika michezo mingine iliyochezwa uwanjani hapo timu ya Proffile iliweza kuifunga timu ya Cuhas kwa pointi 114-39, Cross Over ikaifunga Sengerema kwa pointi 116-41, huku Y. Proffile ikiifunga Oratoria kwa pointi 69-45.