Na Mwamvua Mwinyi
MKUU wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, ametoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuharakisha mchakato wa kuhamia ofisi mpya zilizopo katika eneo la Chicco ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mangosongo alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwani, ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili na kupitia taarifa ya hesabu za Halmashauri.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa miradi ya maendeleo kwa kuanza na uchaguzi sahihi wa maeneo ya utekelezaji ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, sambamba na usimamizi thabiti wa ukusanyaji wa mapato.
Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza viongozi na watumishi wa Halmashauri kwa kufanikisha upatikanaji wa Hati safi, akiwataka waongeze bidii ili kuendelea kuchangia maendeleo ya Wilaya ya Mafia.
Akijibu hoja za Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Juma Salum, alifafanua kuwa ifikapo Septemba 20, 2024, Halmashauri itakuwa tayari imehamia katika ofisi hizo mpya. Hata hivyo, alibainisha kuwa Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi, ingawa waliopo wanafanya kazi kubwa kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa ufanisi.
Salum pia alimshukuru Rais Samia Suluhu H