Timu ya Risasi imeinyoa B4 Mwadui kwa pointi 69-64 katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga na kuifanya itinge nusu fainali ya ligi hiyo inayochezwakwenye Uwanja wa Mwadui, mkoani humo.
Kwa matokeo hayo, Risasi iliongoza katika mzunguko huo kwa pointi 11, ikifuatiwa na Kahama Sixers iliyopata pointi 11, B4 Mwadui pointi 8 na Veta pointi 7.
Akiongea na Mwanasposti kwa simu kutoka Shinyanga, Kamishina wa Ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba, alisema kwa matokeo hayo Risasi sasa itacheza na Veta katika hatua ya nusu fainali.
Simba, alitaja timu zingine zitakazocheza hatua hiyo ni; Kahama Sixers itacheza na B4 Mwadui, akaongeza kusema kuwa mfumo utakaotumikakatika hatua ni wa ‘best of three play off’.