DULLA AOMBA MSAMAHA YANGA SC – MWANAHARAKATI MZALENDO

Msanii wa Singeli, Dulla Makabila ameomba msamaha Yanga kwa kufanya maamuzi ya haraka ya kuhama timu hiyo wakati bado anamapenzi nayo.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Dulla Makabila amepost picha akiwa na Rais wa Yanga, Hersi Said na kuandika ujumbe uliosomeka.

“Leo nilipata bahati ya kukutana na rahisi wa @yangasc kaka angu @caamil_88 kitu cha kwanza alichotaka kujua ni sababu ya mm kuhama team na nilipomueleza alinilaumu sana kwa kufanya maamuzi ya haraka na ya kipuuzi kama yale ile hari mapenzi yangu yapo yanga ila alinielewa na tukaongozana kwenda uwanjani pamoja kutizama mechi ya yanga na nikaokota kwa tajiri Asante rais @caamil_88 kwa upendo ulonionesha.

“Kutokana na kilichotokea baina yangu na yanga naomba nijipe adhabu kwa kufanya show 5 bure kwenye kila sherehe ya yanga na kuokota mipira kwenye mechi 6 za yanga asanteni wana yanga naomba mnipokee kwa mara ya mwisho.”Image

Related Posts