Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Dotto Biteko ameoneshwa kufurahishwa na Kauli mbiu iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri TEF kwa mwaka 2024 iliyokuwa inasema “Uandishi wa Habari Kuhamasisha Matumizi ya Gesi Kulinda Misitu” na kusema imebeba ujumbe unaolenga kuhamasisha matumizi ya gesi kwa kupikia.
Dkt Biteko ameyasema hayo mapema Leo hii April 29 Jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano wa 13 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF uliolenga kujadili mambo mbalimbali ya mabadailiko ya tabia ya nchi.
“Ndugu Mwenyekiti nimefurahishwa na kauli mbiu ya mkutano huu ambayi inasema “Uandishi wa Habari Kuhamasisha Matumizi ya Gesi kulinda Misitu.” Kama ulivyosema kauli mbiu hii inabeba ujumbe unaolenga kuhamasisha matumizi ya gesi kwa kupikia ,kwa lengo la kuokoa misitu yetu nchini “.
Aidha Waziri Biteko amesema kuwa kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa, kwa Ripoti ya tatu ya mwaka 2019.
“Ndugu Wahariri, Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira nchini ya Mwaka 2019, inaonesha kuwa kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa. Hadi kufikia 2015, uzalishaji wa mkaa duniani ulikadiriwa kuwa tani milioni 52 kwa mwaka, na kati ya hizo tani milioni 32.4 zinazalishwa Afrika, ambapo asilimia 42 ya tani hizo zinazalishwa katika ukanda wa Afrika Mashariki unaohusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi. Afrika Magharibi inazalisha asilimia 32, Afrika ya Kati (12.2), Kaskazini (9.8) na Kusini mwa Afrika ni asilimia 3.4.Takwimu hizi zinaashiria hatari kubwa. Misitu inateketea katika ukanda wetu.”
” Wahariri fanyeni jambo. Ungeni mkono juhudi za serikali, vinginevyo kama tusipofanya kitu, nchi yetu itageuka jangwa si muda mrefu na kwa hakika sisi kama Serikali, hatutakubali hili litokee.Katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDG) ya Mwaka 2030, Lengo Na. 7 linaelekeza upatikanaji wa nishati safi na ya bei nafuu. Sisi hapa Tanzania tumebahatika kuwa na gesi ya kutosha. Ndiyo maana “.
“Mhe. Rais Samia amesema tuitumie gesi hii, ambayo ina bei nafuu tuokoe misitu na maisha ya kina mama huko vijijini.Hili la kutumia gesi kama nishati ya kuendeshea magari, sisi kama Wizara tunalipa msukumo mkubwa. Tunajipnaga kujenga vituo vikukbwa vya kusambaza gesi ya magari na Kanuni imeruhusu sasa wenye vituo vya mafuta vya kawaida kuongeza uuzaji wa gesi, hii tukiamini itasaidia kuongeza kasi ya kusambaza gesi ya magari nchini.”
Pia amezungumzia masula ya Uchaguzi ambapo amesema kuwa Mhe Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan amekwisha bayana kuwa nchi yetu itakuwa na Uchaguzi Huru na wa Haki,hivyo Wahariri wahakikishe wanaandika habari za kweli bila kuongeza na uoendeleo wowote.
“Ndugu Waharirir, Hili la maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, taasisi zinazohusika zinaendelea kufanya maandalizi na Mhxeshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekwishasema bayana kuwa nchi yetu itakuwa na UCHAGUI HURU NA WA HAKI. Ombi letu kwenu ninyi Wahariri ni kuhakikisha mnaandika habari za kweli, bila kutia chumvi, kuwa na upendeleo au uonevu kwa mtu au chama chochote cha siasa. Watanzania wanafahamu chama kilichowaletea maendeleo na wanaendelea kuwa na uaminifu mkubwa kwake, hivyo tutashindana kwa haki kabisa.”
“Serikali ina imani ninyi wahariri na waandishi wa habari mtapima kwa haki utendaji wa serikali iliyopo madarakani, mtapima ahadi zinazotolewa na kila upande na uwezekano wa kuzitekeleza, kisha muwasilishe kwa Watanzania nao wapime na kufanya uchaguzi sahihi kwa maendeleo endelevu ya taifa lao. Bila shaka chama kilichofanya vizuri kinafahamika na kitaendelea kufahamika.”
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameomba wahariri kutumia kalamu zao katika kuwatoa hofu wananchi juu ya matumizi ya gesi kwani watu bado wanahofu na kuwapongeza kutumia akili kubwa katika kuipata kaulimbiu hii kwani anaamjni wataitendea haki.
“Katika kutumia kalamu yetu,tungetamani tuone habari nyingi zinazoelezea faida ya matumizi ya gesi ili tuwaondoe Watu wetu hofu ya matumizi ya gesi, Watu bado wana hofu namna ya kutumia gesi. Na kubwa kama mlivyosema muokoe misitu yetu,Itoshe kusema kwa hakika kaulimbiu hii imekuja kwa wakati sahihi na mmetumia akili kubwa kuipata na nina hakika mtaitendea haki”.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bwana Deodatus Balile wakati akisoma Risala yao amesema kuwa wao kama Wahariri wanatamani kuona mchango wa rasilimali gesi katika uchumi wa nchi yetu na watu wake.
“Sisi Wahariri, tunatamani kuona mchango wa rasilimali gesi katika uchumi wa Nchi yetu na watu wake,na zaidi kusaidia Taifa kuondokana na changamoto ya akina mama wenye macho mekundu kutokana na moshi wa kuni kudhaniwa kuwa ni wachawi na kuuwawa katika baadhi Mikoa hapa Nchini. “
Dkt Biteko amemaliza kwa kusema kuwa, Tunafahamu nyakati za uchaguzi baadhi ya watu huwa na tamaa ya kuchezea taarifa na kusukuma habari ‘feki’ kupitia mitandao ya kijamii. Hapa ndipo nataka tushirikiane kwa karibu ninyi wahariri na waandishi wa habari nchini, kuwafundisha hawa vijana na watu wanaoifanya kazi hii kupitia mitandao bila kufahamu maadili ya uandishi wa habari.