BMH YAHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 24 BARAZA LA MAWAZIRI SEKTA YA AFYA EAC

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la sekta ya Afya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Dar es Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku tano, ulioanza leo tarehe 29 Aprili hadi Mei 3, unafanyika kwa njia ya mseto (video na ana kwa ana) umeanza katika ngazi ya wataalam ukilenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 22 wa Baraza hilo.

ambapo taarifa itawasilishwa katika Mkutano wa Makatibu Wakuu.

Mkutano utafuatiwa na ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 2 Aprili 2024, ambapo taarifa itawasilishwa, Makatibu na kuhitimishwa na Mkutano ngazi ya Mawaziri ukaofanyika Mei 3.

Mbali na kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 22 wa Baraza hilo, Mkutano huo utajadili agenda nyingine zinazotarajiwa ikiwemo Mkutano taarifa za Vikundi Kazi (Technical Working Group – TWG) sita (06) vya Sekta ya Afya na mapendekezo ya Tanzania ya kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo, Mganga Mkuu wa Serikali wa Tanzania Prof. Tumaini Nagu, ametoa rai kwa wataalamu wa sekta ya Afya ya EAC kutoa michango itayosaidia Jumuiya kuimarisha miundombinu ya huduma ya afya ili kukabiliana na matishio ya kiafya kwa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

“Tumekuja kujadili na kutoa suluhisho na majawabu yatakayotusaidia kukabili changamoto za kiafya katika Jumuiya yetu kwa kuzingatia ubunifu na weledi katika mifumo yetu ya afya huku tukiwa wamoja na wenye nguvu zaidi” amesema Prof. Nagu

Pro. Nagu amehimiza umuhimu wa Sekta ya Afya katika Jumuiya kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na umoja katika utekelezaji progamu mbalimbali za Afya ikiwemo miradi ya Sekta ya Afya na mikakati inayopangwa ili kufikia mafanikio yanayotarajiwa kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Irene Isaka, ameeleza kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama watapata fursa ya kusikia taarifa zitakazowasilishwa na kila nchi ili kwa pamoja kuweza kuchangia na kushauri namna bora ya kusimamia na kutekeleza programu, miradi na miundombinu ya Afya katika Jumuiya.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu na wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo imewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka.

Wengine kutoka Tanzania walioshiriki Mkutano huo ni pamoja na Wizara za Afya (Tanzania Bara na Zanzibar), Hospitali ya Benjamin Mkapa, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Bohari ya Dawa (MSD), Maabara Kuu ya Taifa, Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria (NAMCP) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA).

Related Posts