BODA BODA CHANGAMKIENI ASILIMIA 10 YA MKOPO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amewahimiza Vijana wanaojishughulisha na Usafirishaji (Boda Boda) kuchangamkia asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri zote nchini ili kuongeza tija na uzalishaji katika kazi zao.

Mhe Ndejembi ametoa wito huo jijini Arusha wakati akihitimisha Mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ambayo yalitolewa kwa boda boda hao na kuwasisitiza kufuata taratibu za kupata mkopo huo ikiwemo kuwa na leseni ya uendeshaji pikipiki.

“ Niwasihi maafisa usafirishaji wote nchini ambao wengi ni vijana kuchangamkia fursa hii ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwenye halmashauri. Mikopo hii imerudishwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi na dhamira yake ya kukuza ustawi wa vijana. Tusimuangushe tutumie fursa hiyo ili kukuza mitaji yetu na kuongeza vipato,” Amesema Mhe Ndejembi.

Aidha, amewasisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama za usalama barabarani ili kuepuka ajali na kuhatarisha maisha yao na abiria wanaowabeba.


Related Posts