RC DANIEL CHONGOLO:HAKUNA ATAKAYEKWEPA MKONO WA DOLA KUHUSU MIMBA ZA UTOTONI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amekemea vikali tabia ya uwepo wa mimba za utotoni hususani wanafunzi katika Wilaya ya Ileje ambapo amesema katika utawala wake hakuna mtu yeyote atakayekwepa mkono wa dola kwa kumpatia mimba mwanafunzi.

RC Chongolo ameyasema hayo  Aprili 28 wakati akiongea na wananchi katika ziara yake eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete wilayani Ileje.

“Niwaambie wala hatutaki kusema mengi ambao wao hawawezi kuacha mabinti wadogo wasome, tutawasaidia kwenda kufanya kazi nyingine zitakazofaa zaidi ili wasionane na mabinti kwa miaka 10,20,25 mpaka 30 ili wakirudi watakuwa walimu wazuri.” amesema Mhe. Chongolo

Mhe. Chongolo anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 4 ndani ya wilaya hiyo.

Related Posts