Baadhi ya Wafanyakazi Kutoka katika Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakimsikiliza muhifadhi akiwapatia historia fupi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Baadhi ya Wafanyakazi Kutoka katika Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakimsikiliza muhifadhi akiwapatia historia fupi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Mkururugenzi wa uendelezaji mifumo ya Tehama Wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mohamed Mashaka ambaye pia ni msimamizi wa mradi wa Tanzania kidigiti akizungumza na waandishi wa habari katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Kutoka kushoto ni Paul Seaden kiongozi wa kikosikazi Kutoka Banki ya Dunia, kushoto kwake ni Mkururugenzi wa uendelezaji mifumo ya Tehama Wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mohamed Mashaka ambaye pia ni msimamizi wa mradi wa Tanzania kidigitali.
Katika picha ni Mratibu wa Mifumo wa Anwani za Makazi Jampyon Mbugi akizungumza na waandishi wa Habari katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Na. Vero Ignatus Arusha
Serikali imezidi kuboresha Huduma za utalii katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kusimika mnara katika mfumo wa kidigital wa 4G katika vijiji vya Nainokanoka,Bulati Irkeepusi na Kitongoji Kidogo cha Alaililai utakaorahisisha watalii kupata huduma mbalimbali haswa upatikanaji wa taarifa ndani ya eneo la hifadhi.
Akizungumza wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya minara ya mawasiliano iliyojengwa kwa ufadhili wa Banki ya dunia, Mkururugenzi wa uendelezaji mifumo ya Tehama Wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mohamed Mashaka ambaye pia ni msimamizi wa mradi wa Tanzania kidigiti amesema Lego kubwa likiwa nikuhakikisha masuala ya utalii yanakuwa kwa kasi sambamba na kukuza uchumi wa nchi.
Mashaka amesema wamekwenda kukagua kazi zinazoendelea katika zinazoendelea katika hilo huku akisisitiza kuwa zote hizo ni jitihada za Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwamba huduma za mawasiliano ziwafikie wananchi popote walipo,Hivyo mwaka 2023 alisaini mkataba kuhakikisha kuwa inajengwa minara 758 ambapo mmoja wapo uliokamilika ni huo wa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.
” Leo hii tumekuja kukagua kazi zinazoendelea katika eneo hii tunakwenda kwa kasi na wenzatu wa Bank ya Dunia wameridhika na kasi tuliyo nayo”alisema Mashaka.
Kwa upande wake Mratibu wa Mifumo wa Anwani za Makazi Jampyon Mbugi amesema kuwa wameanza kushirikiana na Taasisi za Maliasili na Utalii ikiwemo TANAPA,Ngorongoro katika kutoa Anwani katika Mahoteli, maeneo ya vivutio na kuhakikisha kuwa minara yo te inaingia Kenya Mifumo kwaajili ya kurahisisha shughuli za kiutendaji katika maeneo ya Hifadhi
Mbugi amesema Anwani hizi katika maeneo ya hifadhi Zita kuwa na manufaa manakubwa kwani mgeni au mtalii anapotaka kwenda kutalii ataweza kuona umbali wa maeneo atakayofikia, huduma za malazi zilizo karibu, huduma za kibenki au hata sole za matibabu
“Katika eneo hili la Anwani za Makazi wanatoa huduma katila maeneo yote hivyo hata katila eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wamefanya hivyo kwa kutoa mnara wa Mawasiliano”
Akitoa ufafanuzi kwa wawakilishi wa Banki ya Dunia waliotembelea kukagua minara ya Mawasiliano ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Mhandisi Kelvin Mwakaleke Kutoka Wizara ya Mawasiliano. Na Teknolojia ya Habari alisema kuwa happy awali mnara huo ulikuwa unatoa huduma Mfumo wa 2G ilipofika januari 2024 serikali initial fedha kwaajili ya kuuboresha na kuupandisha hadhi kufikia 4G