Wahitimu UDSM Five Class 2007 wanajambo lao

Na Mzandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) five Class 2007 wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam kubadilishana mawazo na kushirikishana fursa mbalimbali za maendeleo.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Aprili 30,2024 jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa wahitimu hao, Frank Gwaluma amesema kikao hicho kitafanyika The Deck Kitchen & Bar iliyopo Masaki karibu na Kambi ya Jeshi Mei 24,mwaka huu.

Amesema lengo kubwa la kikao hicho ni kukumbushana walikotoka na kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kushirikishana fursa za maendeleo.

“Ni kikao cha kawaida tumekiandaa sisi tuliokuwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Facult ya Informatics and Virtual Education (FIVE) kwa sasa College of ICT (CoICT).
“Tukizingatia ni muda mrefu umepita hatujakutana. Hivyo tumeona huu ni wakati muafaka kwetu kujumuika, kufurahi pamoja na kujadiliana fursa za maendeleo, hili ndilo lengo letu hasa.

“Nichukue fursa hii kuwakaribisha wenzetu wote ambao tulisoma pamoja lakini kwa sababu mbalimbali hatuna mawasiliano nao wajue tupo na tunawahitaji sana wajumuike nasi” amesema Gwaluma.

Kuhusu mgeni rasmi, Gwaluma amesema wanatarajia kuwa na baadhi ya walimu waliowafundisha chuoni hapo na humo ndipo atapatikana mgeni maalum.

Related Posts

en English sw Swahili