WAZAZI WANA WAJIBU WA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI, UNYAGO SIO SABABU – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mabalozi wa Amani wa Wilaya ya Tandahimba wamesema tabia ya baadhi ya watu kudhani kwamba suala la kimila la kuwapeleka mabinti unyagoni ndilo chanzo cha mimba za utotoni ni dhana potofu. Wamesema hayo Agosti 31, 2024, wakati wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa dini, serikali za mitaa, wazee maarufu, wakina mama, na vikundi vya ulinzi shirikishi kuhusu kubaini, kuzuia, na kutanzua uhalifu.

Wakati wa semina hiyo, Mabalozi wa Amani walisisitiza kwamba mzazi au mlezi ana jukumu la moja kwa moja katika kulinda na kuongoza watoto, na tabia za jamii hazipaswi kuwa kisingizio cha kushindwa kutekeleza majukumu yao. Waliitaka jamii kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha watoto wanapata elimu ya afya ya uzazi na kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili.

Hii ni sehemu ya juhudi za Wilaya ya Tandahimba kuimarisha usalama na ustawi wa watoto, huku wakilenga kubadili mtindo wa mawazo katika jamii kuhusu masuala ya unyago na mimba za utotoni.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts