Salah adokeza kuondoka Liverpool – Millard Ayo

Mohamed Salah alidokeza huu utakuwa msimu wake wa mwisho ndani ya Liverpool baada ya kufunga bao lake la 15 dhidi ya Manchester United katika ushindi mnono wa 3-0 kwa wageni Old Trafford Jumapili.

Salah amebakiza chini ya mwaka mmoja kutekeleza mkataba wake Anfield na alisema hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika na klabu juu ya kuongeza mkataba wake.

Mmisri huyo amejiandikisha kwenye vitabu vya rekodi vya wababe hao wa Uingereza, akifunga mabao 214 tangu ajiunge nayo mwaka 2017.

“Nilikuwa na msimu mzuri wa kiangazi na nilikuwa na muda mrefu kwangu kujaribu kuwa na matumaini kwa sababu kama unavyojua ni mwaka wangu wa mwisho katika klabu,” Salah aliiambia Sky Sports.

“Nataka tu kufurahia na sitaki kufikiria juu yake. Ninahisi kama niko huru kucheza soka kisha tutaona kitakachotokea mwaka ujao.”

Salah alimtengenezea Luis Diaz mabao mawili kabla ya kuendeleza rekodi yake ya kuwa mfungaji bora katika mechi kati ya United na Liverpool kwa kufunga kwa mechi ya saba mfululizo Old Trafford.

“Kusema ukweli nilikuwa nakuja kwenye mchezo, inaweza kuwa mara ya mwisho (kucheza Old Trafford),” alisema.

“Hakuna mtu katika klabu ambaye amezungumza nami kuhusu mikataba. Sio juu yangu, ni juu ya klabu.”

Salah alisaini mkataba wa miaka mitatu mwaka 2022 ambao uliripotiwa kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, mwenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 18 ($24 milioni) kwa mwaka.

Related Posts