Kinda la Yanga mzuka umempanda Uganda

SIKU chache baada ya kutua na kutambulishwa na klabu ya Wakiso Giants inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda, beki kinda za zamani wa timu ya vijana ya Yanga U-20, Issack Emmanuel Mtengwa amesema uamuzi wa mabosi wa Jangwanui kuamua kuwauza nje wachezaji itasaidia kupata uzoefu na kukua kisoka.

Mtengwa anakuwa mchezaji wa pili kutoka Yanga ya Vijana kusajiliwa kwa mkopo baada ya awali klabu hiyo kumbeba beki wa kati wa timu hiyo ya U20, Shaibu Mtita wiki moja nyuma kabla ya beki huyo wa kulia kujiunga nayo wiki mbili zilizopita.

Mwanaspoti Nje ya Bongo lilimtafuta kinda huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akipata nafasi ya kucheza timu kubwa ya Yanga kwenye baadhi ya mechi za kirafiki.

“Kwanza nimepokelewa vizuri sijakutana na changamoto yoyote kwa kuwa pia nimekutana Mtita ambaye tumecheza Yanga hivyo amekuwa kama mwenyeji wangu,” alisema Mtengwa na kuongeza;

“Kwanza tunawashukuru viongozi wa Yanga timu imekuwa ikiweka utaratibu mzuri kwanza kutupa nafasi ya kufanya mazoezi na timu kubwa ambapo hutujengea kujiamnini lakini hili la kututoa kwa mkopo hilo litasaidia sisi kupata uzoefu na kujulikana zaidi kimataifa.”

Related Posts