Dkt Biteko kumwakilisha rais Samia nchini Namibia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, nchini Namibia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Hydrogen Barani Africa (Global African Hydrogen Summit) Utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 3 hadi 5 Septemba, 2024.

Dkt. Biteko na ujumbe wake wamepokelewa na Balozi wa Namibia Nchini Tanzania, Mhe. Thobias Lebbius akiambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Namibia, Mhe. Caesar Chacha Waitara.

Related Posts