Marekani. Marekani imekamata ndege ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa Dola 13 milioni na kutoroshwa nje ya nchi.
Rais huyo hakuwepo kwenye ndege wakati inakamatwa.
Wizara ya Sheria ya Marekani, imesema ndege hiyo aina ya Falcon 900EX ilikamatwa katika Jamhuri ya Dominika na kuhamishiwa Jimbo la Florida nchini Marekani.
Katika taarifa yake, Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland amesema ndege hiyo, “ilinunuliwa kinyume cha sheria kupitia kampuni ya makombora na kusafirishwa nje ya Marekani.
“Idara itaendelea kufuatilia wale wanaokiuka vikwazo vyetu na udhibiti wa mauzo ya nje ili kuwazuia kutumia rasilimali za Marekani kudhoofisha usalama wa Taifa wa Marekani,” imeandika taarifa hiyo.
Marekani imesema kuwa ndege hiyo ilinunuliwa kutoka kwa Kampuni ya Florida mwishoni mwa 2022 na mapema 2023 na Kampuni ya Shell ya Caribbean ili kukwepa vikwazo.
Hata hivyo, Venezuela imeshutumu ukamataji huo uliofanywa na Marekani ikisema kitendo hicho ni sawa na uharamia.
Endelea kufuatilia Mwaanchi.