Waandishi bunifu nchini, wameombwa kuendelea kuwasilisha miswada kwa ajili ya kushindania Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kwa Mwaka 2024/25 .
Mwenyekiti wa kamati ya Taifa inayosimamia utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Uandishi Ubunifu ya Mwalimu Nyerere Prof. Penina Mlama amezungumza na waandishi wa habari leo Septemba 3, 2024 na kuwaeleza maendeleo ya tuzo hiyo iikiwemo kuendelea kupokea miswaada mbalimbali ya waandishi bunifu nchini.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa, miswada ilianza kupokelewa tangu dirisha tarehe 15 Agosti hadi tarehe 31 Novemba 2024.
Amesema, Tuzo inahusisha nyanja nne za uandishi bunifu ambazo ni Riwaya, Ushairi,Hadithi za watoto na Tamthiliya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo ndio inaratibu Tuzo hiyo ameeleza kuwa, TUZO hiyo ilianzishwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ameeleza lengo likiwa ni kuongeza rasilimali za vitabu na kuwezesha wanafaunzi nchini kupata maandiko mengi ya kusoma na kupata ari ya kusoma vitabu ambayo imepungua.
Washindi katika tuzo hizo watakabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo, mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni 10, Muswada wake utachapishwa na Serikali na kusambazwa shuleni na maktaba za taifa, Ngao na Cheti. Huku mshindi wa pili atapata zawadi Shilingi milioni 7 na cheti, mshindi wa tatu atazawadiwa Shilingi milioni 5 na Cheti.