DK.JAFO :LENGO LA MABADILIKO YA SHERIA YA USHINDANI NI KUMLINDA MLAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akisoma Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024, katika kikao cha 06 ,Mkutano wa 16 Septemba 03,2024, Bungeni Jijini Dodoma.


Wageni mbalimbali waliohudhuria katika usomaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024, katika kikao cha 06 ,Mkutano wa 16, Septemba 03,2024, Bungeni Jijini Dodoma.

Wageni hao ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ndg.Needpeace Wambuya, Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlimuka,, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bw. William Erio na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Wizara hiyo, Dkt.Hanifa Mohamed.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Exaud Kigahe (Mb) wakati wa usomaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024, katika kikao cha 06 ,Mkutano wa 16 Septemba 03,2024, Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika ( Mb) wakati wa usomaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024, katika kikao cha 06 ,Mkutano wa 16 Septemba 03,2024, Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) wakati wa usomaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024, katika kikao cha 06 ,Mkutano wa 16 Septemba 03,2024, Bungeni Jijini Dodoma.

………

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo amesisitiza kuwa lengo la mabadiliko ya sheria ya Ushindani ya mwaka 2024 ni kumlinda mlaji.

Amesema lengo la mabadiliko hayo si adhabu bali ni kuleta hamasa kwa watumiaji ambapo eneo kubwa limeleekezwa kwenye elimu ili watanzania ambao ni walaji waifahamu.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viunga vya bunge mara baada ya kupitishwa kwa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya ushindani ya mwaka 2024.

“Mjadala umekuwa mzuri tumekuwa na muswada wa sheria ya Tume ya Ushindani(FCC) ambao lengo lake lilikuwa ni kumjali mteja hasa upande wamiliki wa hodhi wa soko kutoka asilimia 35 hadi 40,”amesema.

Amesema maeneo mengine yameakisi ni jinsi gani mlaji anapata faida kubwa ili kuhakikisha hazuiwi kupata bidhaa stahiki katika eneo lake bila kudhulumiwa.

Aidha, amesema pia kulikuwa na suala la kupanga kudisplay bei kwa wateja ambapo bunge limeshauri kitumike kifungu cha awali na kutumia utaratibu wa mwanzo bila kuweka adhabu ikiwezekana yafanyike maboresho kwa lengo la kutekeleza sheria kwa ufasaha na wafanyabiashara kuzingatia matakwa ya sheria inavyotaka.

“Tunashukuru maelekezo ya bunge yameena vizuri na muswada umepita hivyo tunasubiri Rais aweze kuusaini ili kuwa sheria kamili.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio amesema hiyo ni ya muda mrefu na kwamba marekebisho hayo yatawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita ya kuvutia biashara na kumlinda mlaji.

“Marekebisho yaliyofanyika ni mengi ikiwemo kubadilisha vifungu vya ushindani, na kuruhusu tume kutoa adhabu katika makosa yanayomuathiri mlaji ambapo vifungu vingine havikuwepo mwanzo, tunaishukuru serikali kwa maboresho haya yakianza kutumika tutatoa elimu ili watu waelewe zaidi,”amesisitiza.

Related Posts