NDEGE YA RAIS YAKAMATWA KWA KUNUNULIWA KINYUME NA SHERIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Marekani imeikamata ndege ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika Jamhuri ya Dominican na kuipeleka katika jimbo la kusini la Florida, ikisema ndege hiyo ilinunuliwa kinyume cha sheria.

 

 

 

 

Rais Maduro ameikosoa hatua hiyo akiita kuwa ni uharamia lakini Marekani imesema ilihitajika kutokana na kukiukwa kwa vikwazo.

 

 

 

 

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na DW, Maafisa wa Marekani wameichukua ndege hiyo ya Dassault Falcon 900EX, ndege binafasi iliyokuwa ikitumiwa na Maduro na wanachama wa serikali yake, huku wizara ya sheria ya Marekani ikisema ndege hiyo ilinunuliwa kinyume cha sheria.

 

 

 

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland amesema katika taarifa kuwa wizara ya sheria ya Marekani imeikamata ndege hiyo wanaoituhumu kwa kununuliwa kwa njia isiyo halali kwa dola milioni 13 kupitia kampuni ya nje ya Venezuela na kutolewa nje ya Marekani kimagendo kwa ajili ya matumizi ya rais Maduro na washirika wake.

 

 

 

Wizara ya mambo ya nje ya Venezuela imetoa taarifa kulaani hatua hiyo ya Marekani kuikamata ndege hiyo.

 

 

 

Tovuti inayofuatilia safari za ndege Flightradar24 imeonesha kuwa ndege hiyo ilisafiri kutokea Santo Domingo had Fort Lauderdale Jumatatu asubuhi.

 

 

 

 

Lakini Jamhuri ya Dominican imesema haikushiriki katika uchunguzi wa Marekani kuhusiana na ndege hiyo.

Related Posts