MARUFUKU WANAWAKE KUZUNGUMZA KWA SAUTI KUBWA HADHARANI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

 

Serikali ya Taliban imeweka sheria mpya iliyopitishwa nchini Afghanistan ambayo inazidi kuibua hisia kali duniani, Vipengele katika sheria hiyo ni pamoja na kupiga marufuku wanawake kuzungumza kwa sauti kubwa hadharani na kuonyesha nyuso zao nje ya nyumba zao.

 

 

 

Sheria hizo mpya tayari zimeidhinishwa na kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Haibatullah Akhundzada.

 

 

 

Wanaume pia hawaruhusiwi kutengeneza nywele zao kwa njia ambayo ni kinyume na sharia.

 

 

Taliban imepiga marufuku vinyozi katika majimbo kadhaa kunyoa au kupunguza ndevu,
ndevu lazima ziwe na urefu wa ngumi.

 

 

 

Sheria ya maadili pia inakataza wanaume kuvaa tai, Wanaume na wanawake pia hawawezi kukaa karibu kwenye gari, matumizi yasiyofaa ya vinasa sauti na redio, kama vile kucheza muziki, ambayo inachukuliwa kuwa haramu.

Related Posts