Ajali ya gari Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera yajeruhi watu 9

Gari ya abiria aina ya Costa yenye namba za usajili T 117 EBP imefeli breki na kugonga gari nyingine aina ya Land cruiser yenye namba za usajili T678 DHM katika eneo la mteremko wa Kashura lililopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kusababisha majeruhi kwa watu tisa.

Baada ya kugonga land cruiser imeparamia nyumba iliyopo karibu na eneo hilo na kujeruhi watu wawili waliokuwa kwenye hiyo nyumba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima amefika eneo la tukio na kueleza kuwa hakuna taarifa ya kifo mpaka sasa na majeruhi hao tisa wamepelekwa hospital ya Rufaa ya Mkoa-Bukoba

Related Posts