TRA punguzaeni migogoro ya kikodi -RC Chalamila

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka TRA kujadili na kupunguza migogoro ya kikodi inayolalamikiwa na Wafanyabiashara, kutanua wigo kwa walipa kodi kulingana na vyanzo vingi vya mapato vilivyopo katika Mkoa na pia kuboresha miundombinu ya kikodi ili TRA iweze kukusanya mapato zaidi.

Chalamila amesema hayo wakati alipokutana na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda akiongozana na baadhi ya Wataalamu wa TRA katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma.

RC Chalamila ameongelea umuhimu wa TRA kurejesha pato lake kiasi kwa ajili ya kuweza kuboresha miundombinu ya kijamii (CSR)kama vile Shule na vitu vinginevyo katika Mkoa huu.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA amemshukuru Chalamila kwa ushirikiano anaoutoa kwa kufanya kazi na TRA na kuthibitisha kuwa Dar es salaam ni kitovu cha biashara kwa kuwa inakusanya kodi zake zote kwa asilimia takribani 80.

Related Posts