Mwenezi CPA Makalla apokelewa mkoani Arusha tayari kwa kuanza ziara yake

Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo Ndugu Amos Makalla amewasili  tayari kuanza ziara yake ya siku 6 katika mkoa wa Arusha na Manyara. makalla amepokelewa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa arusha ndugu loy thomas sabaya pamoja na viongozi wa chama mkoa wa arusha.

CPA Amos Makalla akiwa mkoani Arusha atazungumza na wananchi kwenye mikutano ya nje na mikutano ya ndani yote hii ni kukagua uhai wa chama pamoja na kusikiliza kero za wananchi kisha kuzipatia majibu na atahamia mkoa wa Manyara kwa kuendelea na ziara yake.

Related Posts