MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Kiseo Yusuf Nzowa, akifungua Mkutano wa Kanda ya Kaskazini uliyofanyika mkoani Kilimanjaro, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Fedha, ambapo umehusisha Wakuu wa vitengo vya Usimamizi na Ugavi, Wakuu wa Idara za Mipango, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri, baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, watumishi kutoka Ofisi ya Takwimu Tanzania, wawakilishi kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini Bw. Magai Maregesi, akielimisha washiriki wa mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, waliyoshiriki mkutano huo Kanda ya Kaskazini uliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Pastory Ulimali, akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Takwimu kwa washiriki wa mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa mkutano huo Kanda ya Kaskazini uliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maandalizi ya Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia (PPPC), Bw. Augustino Saibull, akitoa ufafanuzi kuhusu Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na majukumu ya kituo hicho, wakati wa mkutano wa Kikanda, Kanda ya Kaskazini uliyofanyika mkoani Kilimanjaro kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Washiriki wa Mkutano wa Kikanda, Kanda ya Kaskazini, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakifuatilia mkutano huo, uliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Kiseo Yusuf Nzowa (watatu kulia, waliyoketi), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini Bw. Magai Maregesi (wapili kulia waliyoketi), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maandalizi ya Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia (PPPC), Bw. Augustino Saibull (wakwanza kulia, waliyoketi) Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Pastory Ulimali (wakwanza kushoto, waliyoketi) pamoja na washiriki wengine wa mkutano huo mkoani Kilimanjaro.

Picha na Matukio mbalimbali katika Mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kanda ya Kaskazini, uliyofanyika mkoani Kilimanjaro, mkutano huo unafanyika katika kanda zote hapa nchini ambapo kila kanda utafanyika katika mkoa mmoja na kujumuisha washiriki wa mikoa ya Kanda husika.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha – Kilimanjaro)

Na Asia Singano, WF- Kilimanjaro

 

Maafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo ya mabadiliko ya Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuwanufaisha wazawa.

 

Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Kiseo Yusuf Nzowa, wakati akifungua mkutano wa Kikanda, Kanda ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu rasmi zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kanda ya Kaskazini, uliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

 

Aliongeza kuwa kutokana na fursa zilizopo katika Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria hiyo italeta tija endapo watu wanaohusika na masuala ya ununuzi wa Umma wataifuata sheria hiyo na taratibu zote za ununuzi wa Umma.

 

‘’Tumeona mabadiliko mazuri yaliyopo kwenye Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma, ambayo kwa kiasi kikubwa yananufaisha wazawa, wito wangu kwa wanaohusika na manunuzi waifuate Sheria hii’’ alisema Bw. Nzowa.

 

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini, Bw. Magai Maregesi, amewashauri Watanzania kujisajili kwenye mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), ili kunufaika na Sheria hiyo inayotoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wote wakiwamo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

 

‘’ Nawasihi Watanzania kuacha kukwepa Mfumo wa NeST kwa kuwa kuna fursa nyingi kwenye Sheria ya Ununuzi ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, bila kujisajili wazabuni hawatatambua uwepo wao kwa wepesi’’ Alisema Bw. Maregesi.

 

Kabla ya Mikutano ya Kikanda inayoendelea kufanyika, ulianza mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi sahihi ya Takwimu rasmi kwa Wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa, na Waganga Wakuu wa Wilaya Jijini Dodoma hivi karibuni ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck nchemba (Mb).

Related Posts