Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix kwa kushirikiana na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wamezindua rasmi promosheni iliyopewa jina la “AA NA MANOTI” kwa wateja za simu za Infinix.
Promosheni hiyo inalenga kuongeza thamani kwa wateja wa simu za Infinix na hasa kwa wateja wa simu za NOTE 40 na NOTE pro ambazo zilitambulishwa nchini hivi karibuni nchini.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo Alhamisi Aprili 18, 2024 promosheni itafanyika kwa muda wa wiki mbili ikiwawezesha wateja kupata zawadi mbalimbali ikiwamo tiketi ya ndege ya Air Tanzania kwenda na kurudi kwa safari za ndani na nje ya nchi ikiwamo Dubai na China.
Zawadi nyingine ni fedha taslimu Sh2 milioni pamoja na punguzo la bei kwa wateja wa simu za Infinix watakaofanya manunuzi katika muda wa promosheni hiyo ambapo watanunua NOTE 40 kwa 633,000 kutoka bei ya awali ya 680,000 huku NOTE 40 Pro itakuwa 790,000 ikipungua bei kutoka 850,000.
“Lengo letu ni kuendelea kutoa mchango katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kidijitali kwa kuweka mifumo rafiki ikiwamo kukopesha simu janja ambapo mteja anatanguliza aasilimia 30 kama kianzio na kutakiwa kumaliza deni ndani ya miezi mitatu hadi sita,”imesema taarifa hiyo.