Mwenezi Makalla atembelea mpaka wa Tanzania na Kenya ‘Namanga one stop’ aridhishwa kwa kazi

“Nimeridhika na kazi mnayoifanya hapa ‘Namanga One Stop Border Post’ nimejionea foleni ya magari sio kubwa, pamoja na kazi nzuri mnayoifanya endeleeni kuhakikisha suala la foleni linaisha kabisa huku mkiondoa urasimu pamoja na yote muongeze Ushirikiano kwani kwa sasa tupo Vizuri Sisi na majirani zetu wa Afrika Mashariki”.

“Jambo la Mwisho wapeni Ushirikiano hawa wafanyabiashara wa hapa mpakani wasikwame wanapotaka kufanya kazi na kizuri nimeambiwa kiwanda cha Nyama kinafanya kazi”.

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla amesema hayo wakati alipotembelea mpaka wa Namanga leo wakati akiwa kwenye Ziarani Mkoani Arusha.

Related Posts