Hii ni baada ya kutoa msaada wa vyandarua salama katika Hospitali hiyo, inayotoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa Sinza na watanzania wote.
Katibu wa Hospitali ya Sinza Fadhili Kavishe akipokea msaada huo alisema kuwa utaenda kusaidia huduma za IPD- za kulaza wagonjwa.
“Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Sinza, natoa shukrani kwa Meridianbet kwa msaada huu, kama hospitali tumekuwa na mahitaji makubwa kwa kipindi cha nyuma na sasa, tukizingatia Hospitali hivi karibuni imezindua huduma za kulaza wagonjwa (IPD).
“Kwa kiasi kikubwa kuna mahitaji makubwa ya neti kwaajili ya kulaza wagonjwa huku tukiamini kwamba, tuna changamoto kubwa ya ugonjwa wa Malaria katika nchi yetu, kwahiyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kukinga wagonjwa wetu wasiweze kupata ugonjwa huo” Alisema Fadhili Kavishe.
“Tunafahamu ugonjwa wa Malaria ni changamoto kubwa nchini, katika kuhakikisha usalama wa wagonjwa mahospitalini dhidi ya ugonjwa huo, tumeweza kutoa vyandarua mahususi kwa wagonjwa.”