Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Waziri wa Ujenzi,Innocent Bashungwa amewataka Wahandisi kuwajibika katika majukumu pale wanapopatiwa mradi ili kulinda thamani yao.
Akizungumza katika Jukwaa la Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City Waziri Bashungwa amesema Wahandisi ni muhimu katika maendeleo kushindwa kuwajibika katika majukumu yao wanarudisha jitihada zinazofanywa na serikali.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa fursa ya ujenzi wa miradi ambapo wazawa wamepewa kipaumbele.
Waziri Bashungwa alikemea kwa tabia ya baadhi ya Wahandisi ambao, mara baada ya kusaini mikataba na kupokea malipo ya awali hukwepa majukumu yao.
“Kuna wimbi la Wahandisi ambao baada ya kupata (Advance Payment) , wanaanza kusumbua na kushindwa kutimiza ahadi zao,”amesema Bashungwa.
Bashungwa ameitaka bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi ,,(CRB) lazima zisimamie kwa makini tabia na utendaji wake kwa watu hao ili kuepusha ubabaishaji unaoleta hasara kubwa kwa taifa.
Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Said amewataka wahandisi wenzake kutendea haki viapo vyao vya taaluma.
“Wahandisi lazima wawe waadilifu, wafuate uzalendo na kufanya kazi kwa umakini ili kuleta maendeleo ya kweli,”
Amesema kuwa dhamira yake ya kuona wahandisi wanakuwa sehemu ya suluhisho na si tatizo ambapo watakuwa wameisaidia Serikali na maendeleo yakapatikana kutokana na mchango wao.
Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe, amesema mipango ya bodi ni kuimarisha sekta Wahandisi nchini.
“Tumeendelea na mpango wetu wa STEM wa kuhamasisha wanafunzi wa Shule za Sekondari kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza nguvu kazi.
Baadhi ya matukio katika picha katika mkutano wa mwaka kwa Wahandisi, jijini Dar es Salaam.