NIC Insurance yaipiga Jeki Wodi ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili

Mkuu wa Idara ya Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Monica Appolo (kushoto) akimkabidhi Afisa Uhusiano wa NIC Insurance Enfransia Mawala tunzo ya kutambua mchango wa NIC Insurance katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.John Rwegasha (mwenye miwani) akimuonesha moja ya meza na kiti vilivyosadia utendaji katika Wodi ya Watoto jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.John Rwegasha akizungumza kuhusiana na msaada uliotolewa na NIC Insurance katika Wodi ya Watoto katika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
*Dkt.Rwegasha aishukuru NIC kwa kutoa msaada wenye uhitaji.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
NIC insurance imetoa msaada vitu mbalimbali katika wodi ya watoto katika Hospital ya Taifa Muhimbili ikiwa ni kurudisha faida waliopata kwa jamii.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo katika Wodi ya Watoto ya Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa NIC Insurance Karim Meshack amesema uwekezaji wa afya ya watoto ndio maandalizi ya uwekezaji wa nguvu kazi ya Taifa.
Amesema katika NIC kufanya biashara ya Bima na faida iliopatikana wakaona faida hiyo warudishe kwa jamii kuangalia sekta ya afya kwa upande wa afya ya mtoto.
Aidha amesema kuwa irudishaji wa faida kwa jamii kutokana na kuongozwa kwa sera na kupangia mahitaji mahususi ya kwenda kuleta faraja kwa jamii.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa msaada huo ni pamoja ya kuunga jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji huduma katika sekta ya afya nchini.
Hata hivyo amesema watoto wakijengewa mazingira mazuri ya afya ndio maandalizi ya baadae ya kupata viongozi wa kuongoza Taifa letu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.John Rwegasha ameshukuru NIC kwa msaada wao katika Wodi ya Watoto kutokana na kuwepo mahitaji ya msaada huo.
Amesema kuwa k matamanio ya Hospitali hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji Wodi ya Watoto ni kuwa Hospitali ya Taifa ya Watoto.
Amesema kuwa watoto wanahitaji miundombinu mbalimbali ya kuweza kufanya kupata huduma bora za afya.

Related Posts