Kikao cha Mapitio ya Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP)

Kikao cha Mapitio ya Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) kwa kipindi cha Miaka Miwili na Nusu kimefanyika Jijini Arusha kikijumuisha wajumbe kutoka Menejimenti ya Wizara ya Ardhi pamoja na wasimamizi wa Mradi kutoka Benki ya Dunia.

Lengo kuu la kikao hiko ni kupitia na kupima utekelezaji wa kazi za mradi kulingana na makubaliano ya awali kati ya Serikali na Benki ya Dunia katika kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa wananchi.

Akifungua kikao hicho Kamishna wa Ardhi Bw. Mathew Nhonge amesema kwamba kikao hiko ni muhimu katika kupima utekelezaji wa mradi huo kwa kuangalia malengo yaliyowekwa na kiasi gani yamefikiwa . Aidha kikao kitajadili namna ya kuboresha utekekezaji wa mradi ili kufikia malengo kwa wakati.

Kikao hiko ni mwendelezo wa vikao vingi baina ya Wizara na Benki ya Dunia katika kuhakikisha mradi wa LTIP unafikia lengo lake la kuongeza usalama wa milki za ardhi nchini.

Related Posts