Hapi awaonya viongozi wasio wajibika,ataka wasilaumu chama

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi akiwa Kibaha Vijijini amepigilia msumari suala la viongozi waliopo madarakani kuhakikisha wanafanya kazi na kutoa mrejesho kwa wananchi waliompa madaraka hayo kuwaongoza hususani katika kipindi hiki ambacho wataingia katika kugombea nafasi zao na kuomba ridhaa kwa wananchi kuwachagua badala ya kuja kulalamika baada ya kushindwa katika chaguzi.

Hapi alisema katika wakati huu ambao tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa chama hakitaunga mkono wagombea wasiotokana na wananchi ambao watakuwa na wakati mgumu katika kuwatafutia kura

“Hatutaki wagombea wa kuungaunga,tunataka mgombea ambaye wananchi watahitaji awaongoze na ndiyo tutashinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao”alisema Hapi

Hapi amewataka wanaccm na viongozi kujenga utaratibu wa kukaa katika vikao kutatua changamoto zinazowakabili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na chama cha mapinduzi

  

Related Posts