Hapi akemea viongozi kujihusisha na vitendo vya uporaji wa haki za wananchi

Katibu mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi amekema vikali vitendo vya baadhi ya viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yako ya kuwahudumia wananchi na badala yake wanaungana na magenge ya watu wanaopoka haki za wananchi katika maeneo yao jambo linalosababisha chuki kwa chama cha Mapinduzi.

Hapi alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM Kibaha Mjini huku akisisitiza kuwa uhai wa chama cha mapinduzi unabebwa na mambo makuu wawili ambayo ni watu na haki ambavyo kwavyo ndiyo msingi wa chama na ndiyo inafanya wananchi kuendelea kukipenda chama cha mapinduzi

“Mwalimu Nyerere aliwahi kusema msingi wa siasa ni kuwa na watu na Haki,na huo ndiyo msingi wa chama chetu tunapaswa kusimamia haki za watu wetu katika maeneo yao,itashangaza kuona kiongozi anashiriki kukandamiza hali za wananchi huo siyo uongozi unaokubalika ndani ya CCM bali kiongozi wa chama anapaswa kuwa mstari wa mbele kukemea kwa nguvu kubwa ukandamizaji wowote wanaofanyiwa wananchi”alisema Hapi

 

Alisema katika kujenga chama viongozi wanapaswa kutambua chama hicho kimebeba matumaini ya watanzania kwani hakuna chama chenye sera nzuri na muundo mzuri na unaoweza kujali masilahi ya wananchi na makundi yaake kama chama cha mapanduzi lakini mgawqnyiko katika yao unaweza kukibomoa chama ni kuumiza watanzania ambao ndiyo wenye matumaini makubwa na CCM.

“Chama cha Mapinduzi ndiyo kinachobeba matumaini ya wananchi na kuwafanya waishi kwa amani na furaha katika nchi yao lakini Hakuna chama kilichojipanga kulinda tunu ya taifa,kulinda misingi ya umoja na kukataa ukabila na ubaguzi miongoni mwa wananchi”alisema

 

Hapi akatoa Rai kwa viongozi juu ya kufanya kazi kwa kufuata Msingi wa chama cha mapinduzi na kuwafanya wananchi waone umuhimu wa wakikimbilia kwakuwa tunatenda haki nq kuwa daraja kati yao na serikali,

“Haipendezi kufika mahali ukakuta viongozi wanakuwa sehemu ya kuwa walalamikaji juu ya changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao badala ya kuwa watatuzi wa hizo changamoto,niwakumbushe viongozi wa matawi kuwa wanaouwezo na mamlaka ya kuwaita watendaji kuhoji sababu zinazokwamisha usomaji wa taarifa za maendeleo kwa wananchi ili kuondoa malalamiko”alisema Hapi

Hapi alisema Njia pekee ya kuwafanya wananchi waendelee kukipenda chama cha mapinduzi ni viongozi kushughulika na changamoto za watu na kuzifikisha kwa viongozi wanaohusika

Lakini pia aliipongeza jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi kibaha mjini katika kuendelea kuimarisha chama na kuongeza idadi ya wananchama wapya huku ikiendana na malengo ya viongozi wa jumuiya ya wazazi katika kuimarisha jumuiya hii ya wazazi

“Tuache mambo ya mazoea na kupika mihutasiri,katibu wa jumuiya ya wazazi wakae miguu sawa hatuwezi kuwa na katibu asiyefanya vikao katika wilaya yake haikubaliki,lazima kuwe na vikao kujadili ajenda za kudumu kujadili masuala muhimu yanayotufanya kama jumuiya tusonge mbele tufanye kazi”alisema

Related Posts