MFUKO WA UWEKEZAJI WA PAMOJA ‘ALPHA CAPITAL’ WAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI TANZU YA SOKO LA HISA UINGEREZA

MFUKO wa Uwekezaji wa Pamoja wa Alpha Capital umeingia makubaliano na kampuni tanzu ya soko la hisa la Uingereza, Infinitive, kwa ajili ya kupata taarifa muhimu za masoko duniani.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Septemba 7,2024 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Alpha Capital Fund, Gerase Kamugisha, akieleza kwamba Infinitive itatoa huduma muhimu katika kuchambua na kutathmini bidhaa na kampuni zinazohusiana na masoko duniani.

“Kampuni hii inajulikana kwa uwezo wake wa kutoa taarifa kuhusu kampuni zinazozingatia sheria za halal na zile zisizozingatia”.

Kamugisha alisema, “Infinitive itatusaidia kupata taarifa muhimu kuhusu bidhaa na kampuni zinazohusiana na masoko duniani. Hii itatusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu wapi tunaweza kuwekeza ili kupata faida nzuri.”

Aliongeza kwamba baada ya kupata na kuchambua taarifa kutoka Infinitive, Afisa Msimamizi wa Sheria wa Alpha Capital atashirikishwa katika mchakato wa kufanya maamuzi, kuhakikisha kwamba uwekezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni za kisheria na kimaadili.


Related Posts