CHAMA la Mazaltan anayoichezea Mtanzania Enekia Lunyamila limeanza msimu vibaya kwa kupoteza michezo sita kati ya saba iliyocheza ya ligi.
Lunyamila alijiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Eastern Flames iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia na alifunga mabao saba, timu hiyo ikimaliza nafasi ya saba kati ya nane.
Tangu kiraka huyo atambulishwe Mazaltan Agosti 15 mwaka huu, amecheza mechi mbili na mchezo wake wa kwanza alifunga bao lililoipa ushindi na pointi tatu.
Hadi sasa timu hiyo imecheza mechi saba za ligi ikivuna pointi tatu za bao la Mtanzania huyo dhidi ya Necaxa lililoifanya imalize nafasi ya 17 kati ya 18.
Kiungo mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho akicheza dakika 180 za mechi mbili na leo timu hiyo itashuka uwanjani kuumana na America.
Msimu uliopita timu hiyo ilimaliza nafasi ya 14 ikicheza michezo 17 ikishinda minne, sare moja na kupoteza 12.