SERIKALI KUJENGA SHULE 26 ZA WASICHANA ZINAZOTOA MASOMO YA SAYANSI

 

Serikali imeongeza mkazo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.

Hayo yamesemwa hii  na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwenye Marathon ya ERB (Bodi ya usajili wa Wahandisi Nchini)

Waziri Mkenda ameongeza kuwa Serikali imeanzisha Skolashipu kwa wanafunzi wa kidato cha sita watakao faulu vizuri zaidi masomo ya Sayansi
na kwenda chuo kikuu kusoma masomo ya Uhandisi, Tehama, Hisabati na Elimu tiba ambao kupitia ufadhili huo wanalipiwa gharama kwa asilimia mia moja huku lengo la Serikali ni kuchochea wanafunzi wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi.

Profesa Mkenda ameongeza kuwa hakuna Nchi Dunianj inayoendelea bila Sayansi ya Teknolojia hivyo Serikali itaendelea kuongeza nguvu kwenye masomo ya Sayansi ili kupata wanafunzi waliobora kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Lengo la mbio za ERB ni kuwainua na kuwawezesha wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi na kuwezesha, Walimu wanaofundisha masomo ya Sayansi kwa Mkataba.

Huu ni msimu wa kwanza wa ERB Marathon na mbio hizi zitakuwa zinafanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa tisa huku wakimbiaji mia saba na kuendelea wakialikwa kushiriki mbio hizi.

Waziri Mkenda ameweka historia ya aina yake kwa kuweza kumaliza kilomita kumi jambo ambalo limewafurahisha wanariadha wengi zaidi.

Mbio hizo zilianzia katika uwanja wa UDASA kupitia Samu Nujoma, Makomgo juu na mwisho ni katika viwanja vya UDASA vilivyopo katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Related Posts