Aliyekuwa Katibu Mkuu RT Gidabuday afariki dunia

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday amefariki dunia.

Inaelezwa Gidabuday amefariki dunia saa 7 usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 10, 2024 baada ya kugongwa na gari eneo la Maji ya Chai, mkoani Arusha.

Mjumbe wa Riadha kanda ya Mashariki, Alfredo Shahanga ameiambia Mwananchi, kiongozi huyo amefariki baada ya kugongwa kwenye eneo hilo akiwa ameshuka kwenye gari akielekea nyumbani kwake.

“Ni kweli Gidabuday hatunaye,” amesema Shahanga kwa masikitiko.

Shahanga anasema kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, Gidabuday alipoteza maisha hapo hapo baada ya kugongwa.

Endelea kufuatilia Mwanaspoti kwa habari zaidi

Related Posts