CCM YALAANI VIKALI VITENDO VYA KUCHOMWA MOTO MALI ZA KADA WAKE

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed SaID Dimwa,akizungumza na wanachama wa CCM wa Tawi la Mjini Kiuyu mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Maskani hiyo katika ziara ya Sekretarieti ya Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC,CCT Taifa Zanzibar Wilaya ya Wete.

BAADHI ya Wanachama wa CCM Maskani ya Mjini Kiuyu wakifuatilia hotuba ya Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar  Dkt.Mohamed Said Dimwa (Hayupo Pichani )katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akiweka jiwe la msingi Tawi la CCM Mtambwe katika ziara ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar Wilaya ya Wete Kichama.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed SaID Dimwa, akimkabidhi mwanachama mpya  wa CCM kutoka ACT-Wazalendo Khadija Faki kutoka Jimbo la Mtambwe.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed SaID Dimwa,akipokea kadi za ACT-Wazalendo zilizotolewa na wanachama wapya wa CCM kutoka ACT-Walendo kutoka Jimbo la Mtambwe.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote waliohusika na vitendo vya kuchoma moto mali za mwanachama mpya wa CCM kutoka ACT-Wazalendo Salum Mohamed Juma katika shehia ya Wingwi Mapofu Wilaya Micheweni Pemba.

Alisema baadhi ya Wanachama wapya wa CCM wameanza kutishwa na kufanyiwa vitendo vya hujuma na wengine kujeruhiwa na kuharibiwa mali zao hali inayotakiwa kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na usalama haraka.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed SaID Dimwa,mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Maskani ya CCM Mjini Kiuyu Jimbo la Kojani, katika mwendelezo wa ziara ya kikazi ya kuimarisha Chama ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar katika Wilaya Wete Kichama.

Katika usiku wa Augosti 10,2024 watu wasiojulikana wamevamia makaazi mwanachama mpya wa CCM aliyekuwa ACT-Wazalendo Salum Mohamed katika Shehia ya Wingwi Mapofu na kuingia nyumbani kwake wakachoma moto godoro,Vitambulisho,nguo na bendera ya CCM kisha kukimbia baada ya wananchi kujitokeza kuzima moto uliokuwa umeanza kuchoma makaazi ya mwanachama huyo.

Dkt.Dimwa,ameitoa  pole kwa mwanachama huyo na wengine wanaopata changamoto za vitisho na kauli za ubaguzi ambapo amewahakikishia kuwa watakuwa na usalama wa mali na maisha yao ya kila siku.  

“Chama Cha Mapinduzi tuna dhamana ya kulinda amani na utulivu wa nchi kwa gharama yoyote hatuwezi kukubali Zanzibar irudi katika siasa za chuki na machafuko kwa Wananchi wasikuwa na hatia.

Wito wangu kwa vyama vyote vya upinzani tutafakari na kujisahihisha kwa kuacha mara moja siasa za uchochezi zinazoweza kuibua machafuko hivyo tuwe Viongozi wa kuelekeza mema na kudhibiti wafuasi wetu wasifanye vurugu”,alisema Dkt.Dimwa.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kinatarajia vyombo vya ulinzi  na usalama nchini watachukua hatua za haraka kwa kuhakikisha watu wote waliohusika na uhalifu huo bila kujali,cheo,chama cha kisiasa na umaarufu wanafikishwa katika vyombo vya kisheria.

Amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliundwa kwa dhamira ya kumaliza siasa za chuki na visasi ili kuweka nchi katika hali ya Amani na utulivu kwa lengo la kuhakikisha nchi inapiga hatua za kimaendeleo na Wananchi wanaishi kwa amani.

Alisema ni muhimu kila Chama kikajielekeza katika kufanya siasa za ushindani wa sera kwa kueleza na kutekeleza masuala ya maendeleop ili Wananchi wavutiwe na sera kisha wajiunge na Chama wanachoona kinafaa bila kulazimishwa.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, alisema Zanzibar ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Sheria inayoheshimu demokrasia hivyo kila mwanchi ana haki ya kuwa mwanachama wa Chama chochote cha kisiasa.

Mapema Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa,mara baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Mtambwe na amewapokea Wanachama wapya 260 kutoka ACT-Wazalendo Jimbo la Mtambwe Wila ya Wete.

Kupitia mkutano huo amewasihi wanachama wa CCM waliotimiza miaka 18 wahakikishe wanajiandikisha katika zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura ili wawe na kitambulisho cha kupiga kura za ndio zitakazoleta ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa dola.

Related Posts