Madiwani Kasulu sasa wanatumia IPad vikaoni

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma leo Jumanne Septemba 10,2024imetekeleza mpango wa kuhama kutoka katika uendeshaji wa vikao  vya mabaraza yamadiwani kwa kutumia makabrasha na kuanzakutumia vishikwambi.

Ambapo jumla ya vishikwambi 70 vilimenunuliwa na kugawiwa kwa waheshimiwa madiwani,Kamati ya Uinzi na Usalama yaWilaya ya Kasulu,wakuu wa divisheni navitengo pamoja na baadhi ya viongozi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kujadili taarifa za Robo ya Nne yamwaka 2023/2024 Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,  Mhe. Eliya Kagoma amesema kuwa vifaahivyo vitaleta matokeo chanya kwa kurahisishaupataikanaji wa taarifa pamoja na kuokoa fedhazilizokuwa zinatumika kwenye uandaaji wamakabrasha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaWilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba amesema kuwa ugawaji wavishikwambi hivyo ni katika kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za kisereikalizinafanywa kisasa zaidi ili kuwa na halmashauriendelevu inayobadilika kutokana na wakati.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha MapinduziWilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe  amesema jiografia ya halmshauri hiyo ina eneo kubwa la kiutawala hivyo ununuzi wa vishikwambiutapunguza gharama za uendeshaji na fedhazilizokuwa zinatumika kuandaa makabrashazitakwenda kusaidia uetekelezaji miradimingine ya maendeleo.

Diwani wa Viti Maalum kutoka Kata yaNyamidaho, Mhe. Agness Kanyamangengeameipongeza Kamati ya Fedha ya baraza hilokwa kulipitisha jambo ambalo ni zurilitakalopunguza adha kwa wakuu wa divishenina vitengo kusambaza makabrasha kwamadiwani ambapo kutokana na eneo la kijiografia kuwa kubwa fedha nyingi zilikuwazinatumika.

Awali akizungumza katika tukio hilo KatibuTawala wa Wilaya ya Kasulu aliyemwakilishaMkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu amehimiza  suala la umoja namshikamano nchi inapoelekea katika uchaguzipasipo kujali itikadi za kisiasa ili kutimiza azmaya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi.

 

Related Posts