HOMA ya mbio za magari Iringa inazidi kupanda wakati madereva na wasoma ramani wakianza kuwasili leo kabla ya vita ya injini mwishoni mwa wiki.
Kuongezeka kwa dereva mkongwe Himid Mbatta wa Iringa na wakali Altaf Munge, Shehazad Munge na Manveer Birdi kutoka Dar es Salaam kunaweza kumpa wakati mgumu bingwa mtetezi Yassin Nasser ambaye awali alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda mbio hizo.
“Naona kuwepo kwa wakali wote wa mchezo wa mbio za magari mjini Iringa kumeleta msisimko mkubwa na havyo kurudisha nguvu ya ushindano kama ule uliokuwepo miaka ya nyuma,” alidai katibu wa Chama cha Mbio za Magari Iringa (IMSC), Maneno Robert.
Alisema kwamba licha ya kuwepo kwa madereva nguli, ushindani katika mbio za mwaka huu utakuwa mkali kwani wanaoshika nafasi za juu ubingwa wa taifa kina Randeep Birdi wa Dar es Salaam na Gurpal Sandhu wa Arusha pia wapo Iringa kutetea hadhi.
Katibu huyo alisema kila kitu kipo sawa kabla ya mashindano kuanza.
Akifafanua kuhusu ratiba ya mchezo, Robert alisema Jumamosi itaanza na upitiaji wa barabara za mashindano na mchana kutakuwa na ukaguzi wa magari kama yana vigezo vya usalama (scrutineering).
Baada ya taratibu hizo, magari yote yatashiriki katika ufunguzi ambao utaambatana na mbio fupi za uwanjani ziitwazo Super Special Stage.
Baada ya zoezi hilo, magari yatakwenda katika shamba la MT Huwel ambako itafanyika raundi moja ya mashidano itakayojumuisha umbali wa kilomita 26.
“Ni raundi mbili zitaunganishwa ikianza na kilomita 18 na kumalizia na mbio za kilomita nane na huo utakuwa ndiyo mchezo mzima wa siku ya Jumamosi,” alifafanua.
Jumapili barabara za ndani ya Shamba la MT Huwel zitashuhudia madereva wakifanya tena mbio za kilomita 26 ambao zitarudiwa mara kadhaa kabla ya kuwatangaza washindi baada ya kumalizika.
Mashindano pia yanatarajiwa kuwa ni mbio za farasi watatu zikiashiria vita kati ya magari ya Ford Fiesta dhidi ya Mitsubishi Evoluton na Subaru Impreza.
Bingwa mtetezi Nasser na mwenyeji, Ahmed Huwel watakuwa ni viongozi wa timu ya Ford wakati Birdi na Sandhu waliochukua nafasi mbili za juu katika raundi ya ufunguzi mjini Tanga wanawakilisha timu ya Mitsubishi.
Kuna madereva watatu kutoka nje ya nchi kwa mujibu wa Robert.
Ally Katumba ambaye ni msoma ramani wa bingwa mtetezi ni Mganda wakati kutoka Kenya yupo Ravi Chana ambayo atamuongoza Manveer Birdi wa Dar ws Salaam, huku Mzambia Dave Sihoka akimuongoza Gurpal Sandhui wa Arusha.kutoka Dar ws Salaam.
Mzambia Dave Sihoka atamuongoza Gurpal Sandhui wa Arusha.