DC ashtukia uchafu wa mashuka hospitali za umma

Arusha. Serikali imesema itachukua hatua kali dhidi ya wahudumu wa afya watakaoshindwa kudumisha usafi na kusababisha mashuka kutumika yakiwa machafu na kufubaa rangi kwenye hospitali za umma.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga, alisema uchafu kwenye vituo vya afya haukubaliki, na wahudumu wazembe watachukuliwa hatua kali.

Kiswaga ametoa kauli hiyo alipokuwa akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB kwa Hospitali ya Wilaya ya Monduli.

Msaada huo utaboresha huduma kwa wagonjwa hasa baada ya serikali kutumia zaidi ya Sh500 milioni kukarabati majengo na kujenga majengo mapya matano kwa ajili ya huduma mbalimbali. Maboresho haya yameongeza idadi ya wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa.

Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali NMB, Vicky Bishubo amesema lengo la msaada huo ni kurahisisha utoaji wa huduma za afya.

Vifaa vilivyotolewa vikiwa na thamani ya Sh6.5 milioni ni pamoja na mashuka, vitanda na viti mwendo.

Related Posts