MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Mang’una anasema kuwa kumekua na ongezeko la wananchi la kuwapeleka watoto hospitali kupata matone ya vitamin D.
Ongezeko hilo linatokana na kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wananchi juu ya umuhimu wa vitamin D kwa watoto chini ya miaka mitano, jambo ambalo limechangia wazazi kuwapeleka hospitali kupata matone hayo.
Mwaka 2021, Serikali ilizindua Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ambayo inahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miaka sifuri hadi minane.
Katika programu hiyo, serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imekua ikitekeleza afya Tano za lishe, afya, elimu, ulinzi na usalama na malezi yenye mwitikio.
Awali, Dk. Mang’una amesema kuwa sekta binafsi imekua na mchango mkubwa katika kuhamasisha na kushiriki kwenye zoezi la utoaji wa matone ya vitamin D, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa mwamko wa wazazi wanaowapeleka watoto hospitali kupewa matone hayo.
Akizungumza hivi karibuni, Dk Mang’una anasema kuwa, Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wadau mbalimbali Ili kuhakikisha kuwa zoezi la utoaji wa matone ya vitamin D linafanikiwa kuliko hapo nyuma
” Tumekua tukishirikiana na sekta binafsi kutoa elimu kwa jamii ya umuhimu wa vitamin D kwa watoto chini ya miaka mitano, lakini pia tumeanzisha kamati za afya kuanzia ngazi ya kata ambapo Ofisa afya na Ofisa Lishe wanapatikanna ili kutoa elimu kwa wananchi,” amesema Dk. Mang’una.
Dk. Mang’una amesema wadau hao Kwa pamoja wamekuwa walitoa elimu ya umuhimu wa vitamin hiyo Kwa mtoto toka anapokua tumboni Ili mama mjamIto aweze kula chakula vyenye virutubisho ambayo vitasaidia kutengeneza vitamin D Kwa wingi.
Anasema kumekua na tafiti nyingi ambazo zinaonyesha kuwa, magonjwa mengi ya watoto yanatokana na upungufu wa vitamin D, sio tu mifupa kuwa dhaifu, lakini mtoto anaweza kuzaliwa na uzito pungufu, usonji, kupata maambukizi ya virusi na bakteria, saratani, magonjwa ya moyo na hata mama mjamzito kupata kifafa cha mimba.
“Mtoto anapozaliwa kuna kiasi cha vitamin D kinahitajika ambacho linatokana kwa mama yake na nyingine ataipata kwa njia ya kunyonyeshwa kuimariaha ukuaji wa afya yake ya mwili na ubongo, madhara ya mtoto kukosa vitamin D ni pamoja na udumavu, mifupa yake kuvunjika mara kwa mara, kupata maambukizi ya virusi na bakteria, kifua na matatizo mengine ambayo yatarudisha nyuma ukuaji wake.
Ameongeza baadhi ya watoto wanaanza kuonyesha dalili wakiwa na miezi sita na kuendelea mwili dhaifu, wana matege, ngozi dhaifu,wanaumwa mara kwa mara na hata baadhi yao kupata upungufu wa damu na mtoto anapotimiza umri wa mwaka 1-3 anahitaji kupata vitamin D ya kutoaha ili aweze kukua katika hali ya utimilifu, samaki
Kwa upande wake Ofisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe nchini (TFNC), Doris Katana amesema kuwa siku 1000 ambazo huhesabiwa tangu siku mimba inapotungwa hadi mtoto anapotimiza miaka 2 ni siku muhimu kwa mama mjamzito na mtoto kula vyakula vyenye virutubisho ii kumjenga mtoto asiweze kuzaliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwamo ukosefu wa vitamin D ambayo pia unaweza kupatikana kwenye samaki.
Amesema kuwa, mtoto anapotimiza umri wa miezi sita anaanza kula vyakula mchanganyiko huku akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama, hivyo basi anapaswa kutengenezwa vyakula vyenye virutubisho vyote ikiwamo samaki kwa wingi ili aweze kuimariaha afya yake.
Amesema kuwa mtoto anapokosa lishe bora kuanzia tumboni madhara yake ni makubwa ambapo anaweza kupata Utapiamlo, upungufu wa vitamin D mwilini ambayo unaweza kumsababishia kupata ulemavu na madhara mengi.
Tafiti zinaonyesha lishe bora katika kipindi maalum cha Siku 1000, inaokoa maisha ya watoto zaidi ya milioni moja kila mwaka na uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyoambukiza kama kisukari, saratani na magonjwa ya moyo ukubwani.
“Ni muhimu jamii kujali afya ya mama wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha kwa afya ya mtoto wake, lishe bora na mazingira safi na kuishi bila msongo wa mawazo ili kuboresha ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili lakini pia hisia za mtoto zinachangiwa na lishe ya mama na maisha anayopitia wakati wa ujauzito,” amesema.
Ameongeza madhara ambayo anaweza kupata mama mjamzito au mtoto ndani ya sku 1000 ni pamoja na upungufu wa Vitamin D mwilini, upungufu wa wekundu wa damu, ukosefu wa madini joto na kutokuongezeka uzito.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na watoto wenye ulemavu ya Kaya Foundation,Anapili Ngome amesema kuwa, miaka iliyopita watoto wengi wanaozaliwa na ulemavu jamii imekua ikiwanyanyapaa na kuwaona kuwa hawana haki katika jamii zao, hali ambayo Kwa sasa ni tofauti, jamii imeanza kuwa na mwamko.
” Taasisi yangu inajishughulisha na watoto wenye vichwa vikubwa na walemavu ambao wamekuwa wakinyanyapaliwa na jamii kutokana na changamoto walizonazo, kitu ambacho sio sawa, watoto hawa wananyimwa haki ya kulelewa, kupata matibabu, elimu na huduma nyingine katika jamii.
“Kwasasa hali ni tofauti kidogo, wazazi wameanza kuwa na uelewa na kuanza kuwapa haki zao za msingi ikiwamo malezi bora, elimu na matibabu pale wanapougua au kupata changamoto za kiafya,”amesema Ngome.
Ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali pamoja na wadau wanapaswa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi Ili waweze kuwatoa, kuwapa elimu na hata wanapoumwa kuwapeleka hospitali kupata matibabu”, amesema Ngome.
Baadhi ya wananchi wamedai kuwa, elimu ya afya ya uzazi inayotolewa na Serikali Kwa kushirikiana na wadau wengine inasaidia kuqafikia wananchi Kwa haraka na kuona umuhimu wa vitamin hiyo kwa mtoto.
” Kamati za afya za mtaa zinashurikiana na Ofisa Lishe kata na Ofisa afya kata kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa vitamin D kwa mtoto, jambo ambalo limesaidia kuongezeka Kwa uelewa kwa wananchi na wazazi kwa ujumla.
” Serikali inapotoa tangazo la kutolewa kwa matone ya vitamin D tumekuwa tukihamasisha Ili watoto wenye umri chini ya miaka mitano kupelekwa kwenye vituko tajwa ili waweze kupewa matone hayo,” amesema Joseph Shukrani mkazi za Mwananyamala.
Naye mkazi mwingine wa Kinondoni, Imani Hamza amesema kuwa, siku hizo wanaume wanabeba watoto kuwapeleka kwenye chanjo au kupata matone ya vitamin D mara baada ya tangazo kutolewa.
” Uko nyuma hayo mambo yalikua hayapo, lakini siku hizi, sisi kina baba tumekua tukiwapelaka watoto kliniki kupata chanjo au kuwapeleka kupata matone ya vitamin D mara baada ya kutolewa kwa tangazo, hii inatokana na mwamko uliopo ambao umesaidia kuongeza hamasa ya malezi ya watoto Kwa wazazi wote wawili ( baba na mama),” amesema Hamza.