Jesca afunika kwa asisti | Mwanaspoti

DB Troncatti imebakiwa na michezo miwili ili ikamilishe michezo 30 ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu (BD), huku mchezaji wa timu hiyo, Jesca Lenga akifunika kwa kutoa asisti 214.

Nyota huyo anafuatiwa na Tukusubila Mwalusamba wa Tausi Royals aliyeasisti mara 135, huku Noela Renatus wa Vijana Queens akishika nafasi ya tatu asisti 103. 

Wachezaji wengine ni Tumwagile Joshua (DB Troncatti) asisti 94, Nasra Bakari (DB Troncatti) 84 na Irene Kapambala (Polisi Stars) 82.

Wengine ni Maria Boniventure (Pazi Queens) 82, Juliana Sambwe (Tausi Royals) 81, Rehema Silomba  (DB Lioness) 80 na Faraja Mhomisori (Jeshi Stars) 74.

Kwa upande wa uzuiaji (blocks), mchezaji Beatrice Akyoo wa timu ya Twalipo Queens anaongoza kuzuia  mara 82.

Block inahesabika pale mchezaji anapozuia mpira wa juu kwa mchezaji wa timu pinzani bila ya kufanya madhambi.

Wachezaji wengine waliofuatia ni Irene Kapambala (Polisi Stars) 80, Neema Yakobo (Vijana Queens) 62 na Anamary Cyprian (Jeshi Stars) 51.

Related Posts