WAKAAZI WA KATA YA KIGHARE WAGUSWA NA MCHANGO WA VIFAA VYA ELIMU

Wakaazi wa Kata ya Kighare Wilayani Mwanga leo Aprili 30, 2024 wamepokea kwa furaha mchango wa vifaa pamoja na fedha taslimu kwa ajili kuboresha maendeleo ya utoaji wa elimu katika shule ya msingi Kilaweni.

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kompyuta mpakato mbili (Laptop), Printa (1) na fedha taslimu shilingi milioni moja.

Akizungumza kwa furaha baada ya kupokea Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kilaweni Bw. Aman Mbwambo amesema kuwa kupatiwa vifaa hivyo kutakwenda kusaidia kuongeza ufanisi zaidi katika shughuli mbalimbali za kitaaluma katika shule hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Bw. Dhahiri Mziray amebainisha kuwa upatikanaji wa vifaa hivyo na fedha zilizotolewa ni chachu ya kuongeza maendeleo ya ushindani wa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Kilaweni.

Awali wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mwakilishi wa mlezi wa Shule ya Kilaweni Bw. Said Sultan amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ambazo zimekuwa ni kuhakikisha shule zote nchini zinapata mahitaji ya vifaa muhimu vitakavyowezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora ili kukuza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Ugawaji wa vifaa vya elimu pamoja na fedha taslimu shilingi milioni moja umetolewa na Mlezi wa Shule ya Kilaweni Bw. Said Mndeme ambaye pia Mkurugenzi wa Miliki kutoka TBA.





Related Posts