Mkilipa $44 mtatibiwa hapa Lumumba Zanzibar

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Saada Mkuya amekagua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume (AAKIA) Visiwani Zanzibar ikiwa ni hatua ya kutekeleza Utaratibu wa Ulipaji wa Bima ya Lazima kwa mtalii ambapo Gharama yake ni $44

Mkuya amefikia hatua hiyo ya kwenda kujionea namna watalii wakiingia Zanzibar na kuhakikisha mtalii yeyote anaingia Zanzibar awe na bima sambamba na kujionea miundombinu ya kutekeleza zoezi hilo la bima visiwani humo.

katika hatua nyingine waziri wa fedha ametembelea Hospitali ya serikali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini ya Lumumba ambayo ni mpya na yenye vifaa vyote vya kisasa inayosimamiwa na madaktari wa kigeni Hopsitali hiyo imepangwa kutumika kwa watalii ikitokea wamekutwa na majanga.

Related Posts